Wanasayansi nchini Canada na Marekani wamechapisha utafiti ambao unakosoa nadharia ya sasa kuhusu asili ya mwanadamu wa sasa kwamba anatokea katika Bara la Afrika.
Wakiangalia katika data za urithi, watafiti hao kutoka Chuo kikuu cha McGill na Chuo kikuu cha California – Davis wanasema kulikuwa na watu wengi waliokuwa wanaishi katika sehemu nyingi za Afrika, ambao walihamia kutoka sehemu moja kuelekea nyingine na kuchanganyikana kwa zaidi ya miaka maelfu kadhaa iliyopita.
Matokeo haya ya utafiti yanakinzana na nadharia kwamba binadamu wa sasa- Homo Sapiens ni kizazi cha mababu waliokuwa wakiishi Mashariki na Kusini mwa Bara la Afrika.
“Katika vipindi tofauti, watu walikubaliana na nadharia kwamba asili ya Homo Sapien inaonyesha kuwa binadamu kwanza walitokea mashariki au Kusini mwa Afrika,” alisema Brenna Henn, mtaalamu wa urithi katika chuo kikuu cha California, Davis ambaye pia ni mwandishi mkuu mwenza wa utafiti.
“Lakini imekuwa vigumu kukubaliana kuhusu nadharia hizi kutokana na uchache wa mabaki ya watu wa kale na rekodi za kiakiolojia za binadamu ambazo zinaonesha kuwa Homo Sapien walipatikana wakiishi kote barani Afrika kwa walau miaka 300,000 iliyopita,” alisema