ZINAZOVUMA:

Iran: Uchaguzi ndani ya siku 50 zijazo

Msemaji wa Baraza la Kulinda Katiba ya Iran Dkt. Hadi...

Share na:

Dkt. Hadi Tahan Nazif, Msemaji wa Baraza la Kulinda Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema baraza maalumu litaundwa kuandaa mazingira ya kufanyika uchaguzi wa urais katika kipindi cha siku 50 zijazo.

Msemaji huyo wa Baraza la Kulinda Katiba ya Iran amesema kuwa baraza hilo maalum litajumuisha Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge), Mkuu wa Idara ya Mahakama na maafisa wengine wa ngazi za juu wa serikali ya Jamhuri hiyo ya Kiislamu.

Amesema kwa mujibu wa Katiba, Mohammad Mokhber, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ndiye atakayekaimu nafasi ya Rais Ebrahim Raisi altefariki katika ajali ya helikopta jana Jumapili.

Amesema Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ataiongoza serikali akisha apasishwa, na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya