ZINAZOVUMA:

TCRA washtukia katuni za watoto, waja na hii

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imesema itashirikiana na mzalishaji binafsi...

Share na:

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imesema itashirikiana na mzalishaji binafsi kutengeneza katuni za watoto ili kudhibiti maudhui yasiyofaa kwa watoto yanayoruka kwenye runinga.

Suala la kuwepo kwa katuni zisizoendana na maadili ya Kitanzania limekuwa likiibuka na kuzua minong’ono miongoni mwa watu huku TCRA ikirushiwa lawama kwa kutodhibiti maudhui hayo.

“Katika suala la katuni zisizofaa kwa watoto, TCRA tutashirikiana na mzalishaji binafsi ili kuzalisha katuni zenye viwango vya juu kwa ajili ya watoto, vilevile tunarekodi michezo ya kitamaduni ya makabila 120 ambayo nayo itakuwa katika ubora wa hali ya juu,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt Jabiri Bakari katika taarifa ya mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari.

Dkt Jabiri alisema majukumu ya TCRA ni zaidi ya zaidi ya kuwezesha huduma za matangazo kwani mamlaka hiyo inajukumu la kuhakikisha maudhui yanayorushwa yanafuata maadili ya uandishi wa habari, yanazingatia sheria za nchi, kulinda maadili na urithi wa Taifa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya