ZINAZOVUMA:

Ukraine yamfuta kazi Waziri wa Ulinzi

Raisi wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametangaza kumfuta kazi Waziri wa...

Share na:

Raisi wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametangaza kumfuta kazi Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Bw. Oleksii Reznikov.

Reznikov amekuwa kiongozi wa Wizara hiyo kabla ya kuanza kwa uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 2022.

Katika hotuba yake Rais Zelenskiy amesema ni wakati wa utekelezaji mbinu mpya katika Wizara ya ulinzi ambazo zitamuhitaji mtu mwingine atakaeiongoza mipango ya Wizara hiyo.

Aidha Rais Zelenskiy amempendekeza Rustem Umerov ambae ni msimamizi wa hazina inayoendesha Mali ya Taifa nchini Ukraine kuchukua nafasi ya Wizara ya Ulinzi.

“Ninaamini kuwa wizara inahitaji mbinu mpya na mifumo mingine ya mwingiliano na wanajeshi na jamii kwa ujumla,” Rais wa Ukraine alisema katika hotuba yake kutoka mji mkuu wa Kyiv.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,