Muungano wa Azimio La Umoja nchini Kenya unaoongozwa na Raila Odinga unakusanya ushahidi wa kuwasilisha katika kufungua kesi katika Mahakama ya Jinai ya Kimataifa ICC.
Kesi hiyo itakuawa dhidi ya polisi wa Kenya kwa kosa la kutumia nguvu kupita kiasi katika kukabiliana na raia, wakati wa Maandamano ya kupinga kuongezeka kwa gharama za maisha nchini humo.
Utumiaji wa nguvu kupita kiasi unatajwa kusababisha vifo na majeruhi kadhaa, hivyo upinzani unatarajia kupelekea malalamiko yao kwa Jumuiya za Kimataifa kutazama kwa makini matukio yanayoendelea nchini Kenya hasa namna ambavyo Polisi wanashughulika na waandamanaji wanaotimiza haki yao ya kiraia ya kukusanyika kwa amani
Aidha, kesho Julai 25, 2023 viongozi wa Azimio watakutana kukagua ushahidi uliokusanywa hadi sasa kabla ya maandamano ya Jumatano, Julai 26, 2023