ZINAZOVUMA:

UN: Miaka 14 ya vita, bado hali tete Syria

Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria vina zaidi ya...

Share na:

Maafisa wanaoratibu hali ya kibinadamu Syria wanakadiria watu milioni 16.7 wanahitaji misaada ya kibinadamu

Wakati Syria inaingia mwaka wa 14 katika vita vya wenyewe kwa wenyewe bila ya suluhisho la kisiasa, mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifayaziomba jumuiya za kimataifa kukumbuka madhila ya mamilioni ya watu wanaoendelea kuteseka kutokana na vurugu, uharibifu na manyanyaso.

Miaka kumi na tatu ya mgogoro imesababisha idadi isiyofikiriwa ya vifo kwa watu wa Syria, na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaonya kuwa mgogoro huo unaendelea kusababisha maafa kwa raia na kuifanya hali kibinadamu ambayo ni mbaya kuwa kuzorota zaidi.

Katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka hii mibaya, Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu nchini humo, Adam Abdelmoula na Mratibu wa Kikanda wa Misaada ya Kibinadamu kwa Mzozo wa Syria, Muhannad Hadi walitoa taarifa ya pamoja siku ya Ijumaa wakionya kuwa kiwango cha mahitaji hakijawahi kuwa juu kama ilivyo sasa.

Wanakadiria kuwa watu milioni 16.7 wanahitaji misaada ya kibinadamu, wengi wao wakiwa waathirika wa tetemeko baya la ardhi la mwaka jana, ambalo limesababisha mgogoro ndani ya mgogoro.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya