ZINAZOVUMA:

Ugonjwa wa shinikizo la damu umeongezeka Tanzania

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa shinikizo la...

Share na:

Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu umeongezeka kutoka wagonjwa 688,901 kwa mwaka 2017 hadi kufikia wagonjwa 1,345,847 kwa mwaka 2021 sawa na ongezeko la 95.4% katika kipindi hicho cha miaka Mitano.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameyasema hayo Jana alipotoa tamko kwa Waandishi wa habari katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma ikiwa ni madhimisho ya Siku ya Shinikizo la Juu la Damu duniani.

“Takwimu hizi zinatuonesha kwamba wagonjwa hawa wenye shinikizo la damu wameonekana kuongezeka takribani mara mbili zaidi kwa kipindi cha miaka mitano.” amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amesema kwa ujumla magonjwa yasiyoambukizwa yameongezeka kwa 9.4% kwa kipindi cha miaka mitano kutoka mwaka 2017-2021 kwenye vituo vya Afya chini, wagonjwa hawa wameongezeka hadi kufikia wagonjwa 3,440,708 kwa mwaka 2021.

Pia, ameongezea kwa kusema kuwa takwimu zinaonyesha watu 3-4 kati ya 10 wana shinikizo la juu la damu kwa uchunguzi uliofanywa katika jamii kwenye mikoa ya Pwani, Arusha, Geita, Mtwara, Lindi, Zanzibar, Iringa na Dares Salaam.

Kwa upande wa dawa, Waziri Ummy amesema Wizara imeruhusu dawa za kukabili shinikizo la juu la damu katika ngazi ya msingi kwa kuruhusu dawa tatu (3) ambazo ni Losartan, Amlodipine na Hydralazine kutumika katika ngazi ya kituo cha afya na dawa mbili (2) ambazo ni Nifedipine na Frusemide ambazo hutumika katika ngazi ya zahanati.

Mpango wa Serikali kupitia Wizara ya Afya ni kutoa mafunzo ya utoaji wa huduma za magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo huduma za ugonjwa wa shinikizo la damu kwa watoa huduma 2400 kutoka vituo vya Afya vyote 600 katika mikoa yote 26.

Mwisho, Waziri Ummy amewakumbusha Watanzania juu ya umuhimu wa Kubadili mtindo wa maisha kwa kuzingatia ufanyaji wa mazoezi, kuepuka tabia bwete, kuepuka matumizi ya tumbaku na bidhaa zake na kupunguza matumizi ya vilevi.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya