ZINAZOVUMA:

Ufaransa yazuia wanafunzi kuvaa abaya shuleni

Wizara ya elimu nchini Ufaransa imepiga marufuku vazi la abaya...

Share na:

Serikali nchini Ufaransa imetangaza marufuku kwa wanafunzi wa kike wa shule za umma kuvaa vazi aina ya abaya ambalo huvaliwa mara nyingi na waumini wa dini ya Kiislamu nchini humo.

Marufuku hiyo itaanza Septemba 4, 2023 baada ya muhula mpya wa masomo wa nchi hiyo kuanza rasmi.

Hatua hiyo inakuja baada ya Ufaransa kupiga marufuku alama za kidini katika shule za serikali na majengo ya serikali, ikisema kwamba zinakiuka sheria za kilimwengu.

Hata hivyo, nchini humo kuvaa hijab kwa msichana katika shule za Serikali kumepigwa marufuku tangu 2004 katika shule zinazomilikiwa na serikali.

Aidha hatua hii ya sasa imejiri baada ya miezi kadhaa ya mjadala kuhusu uvaaji wa abaya katika shule za Ufaransa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya