ZINAZOVUMA:

Uchunguzi unaendelea ‘Hoteli’ nne kuungua Zanzibar

Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wa Kusini Unguja...

Share na:

Hoteli nne na nyumba moja ya makazi zimeungua moto Paje Wilaya ya Kusini Unguja, Mkoa wa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Hoteli hizo ni pamoja na Cristal resort, Maisha Matam, Drifters na The Nest Boutique resort

Mkuu wa Wilaya hiyo na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, Rajab Mkasaba ameeleza kuwa tukio hilo limetokea saa 6:00 usiku wa kumkia Jana Julai 9, 2023.

“Kuna hoteli nne na nyumba moja ya kulala wageni hapa Paje zimeungua sehemu ya reception (mapokezi) kutokana na moto, baadhi ya wafanyakazi wanasema moto umeanzia jikoni lakini bado uchunguzi unaendelea,” amesema Mkasaba

Amesema hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hiyo na kwamba moto huo umeenea kwenye hoteli zote hizo kwasababu ya upepo na ikizingatiwa zimeezekwa kwa makuti.

Mkasaba amesema wananchi kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto wamefanikiwa kuzima moto huo bila kuleta madhara zaidi.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,