ZINAZOVUMA:

Uchaguzi wa kwanza Sudan Kusini kufanyika mwakani

Raisi wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema kuwa uchaguzi uliocheleweshwa...

Share na:

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amesema uchaguzi ambao ulichelewa kwa muda mrefu nchini humo utafanyika mwakani kama ilivyopangwa.

Hata hivyo Rais Kiir amesema atawania tena uchaguzi huo, wa kwanza tangu nchi hiyo kupata uhuru.

Mpaka sasa hakuna mgombea mwingine ambaye ametangaza kugombea lakini Makamu wa Kwanza wa Rais, Riek Machar ni miongoni mwa wanaoanatarajiwa kutangaza nia ya kugombea kinyang’anyiro hicho.

Rais Kiir amekuwa katika nafasi hiyo tangu uhuru wa nchi hiyo mwaka 2011 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu.

Hata hivyo mzozo uliendelea hata baada ya uhuru. Vita vya wenyewe kwa wenyewe viliibuka tena mwaka 2013 wakati rais Kiir alipokosana na Machar.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya