ZINAZOVUMA:

Ubalozi wa Marekani watoa tahadhari kwa raia wake waliopo Kenya

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umetoa ushauri kwa raia wake...

Share na:

Ubalozi wa Marekani umetoa ushauri wa kiusalama kwa raia wake waliopo nchini Kenya kabla ya kufanyika tukio la kuwakumbuka watu waliofariki wakati wa maandamano lilipangwa kufanyika na Muungano wa Azimio la umoja.

Katika taarifa yake, ubalozi huo umeonya kuwa matukio hayo yanayotarajiwa kufanyika kote nchini humo yanaweza kugeuka kuwa ghasia licha ya hakikisho kutoka kwa upinzani kwamba yatakuwa ya amani.

Ubalozi wa Marekani umewashauri raia wake kuepuka maeneo ambayo matukio ya kumbukumbu yatakayoambatana na matembezi yatafanyika, kufuatilia vyombo vya habari vya ndani kwa ajili ya kupata taarifa, na kuepuka mikusanyiko ya watu.

“Hatua za kuchukua ni pamoja na kufahamu mazingira yako, kukagua mipango yako ya usalama wa kibinafsi na kubeba Kitambulisho sahihi”, ilieleza taarifa ya ubalozi.

Muungano wa Azimio unaoongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga unatarajiwa kufanya kumbukumbu nchini humo kwa heshima ya Wakenya waliopoteza maisha yao wakati wa maandamano ya kuipinga serikali yaliyoandaliwa wiki zilizopita.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,