ZINAZOVUMA:

Tunisia na Umoja wa Ulaya wakubaliana kudhibiti uhamiaji haramu

Umoja wa Ulaya umesaini makubaliano ya kimkakati ya kumsadia Tunisia...

Share na:

Tunisia na Umoja wa Ulaya wamesaini makubaliano ya “ushirikiano wa kimkakati” ambao unajumuisha kupambana na wasafirishaji wa binadamu na kuimarisha usalama kwenye mipaka.

Hayo yamekuja wakati kuna ongezeko kubwa la boti za wahamiaji zinazosafiri kutokea taifa hilo la Afrika Kaskazini kuelekea Ulaya.

Makubaliano hayo yanafuatia wiki kadhaa za mazungumzo na Umoja wa Ulaya ambao uliahidi msaada mkubwa kwa Tunisia wa euro bilioni 1 kusaidia kufufua uchumi wa Tunisia unaodorora, kuokoa fedha za serikali na kukabiliana na mzozo wa wahamiaji.

Fedha nyingi kati ya hizo zitatumiwa kufanya mageuzi ya kiuchumi ambapo.

Aidha Mkuu wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen alisema jumuiya hiyo itatoa euro milioni 100 kwa Tunisia kusaidia kupambana na uhamiaji haramu.

Makubaliano hayo yanaimarisha uthabiti wa uchumi, biashara na uwekezaji, matumizi ya nishati ya kijani na uhamiaji halali.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya