Raisi wa zamani wa marekani Donald Trump amefunguliwa mashtaka na jopo la wazee wa mahakama katika mahakama ya Manhattan jijini New York, Marekani.
Trump anatuhumiwa kumlipa pesa haramu mwanamke alieshiriki nae kitendo cha ngono mwaka 2006 na kumtaka akae kimya.
Baada ya uchunguzi kufanyika Trump amekutwa hatiani baada ya kumlipa pesa mwanamke huyo. (Jina lake tunalihifadhi).
Tukio hilo limetishia malengo yake ya kutaka kugombea tena nafasi ya uraisi 2024 kama alivyotangaza kuwa angegombea tena, lakini pia tukio hili linamfanya kuwa Raisi wa kwanza katika Taifa la marekani kushtakiwa.
Aidha Trump amelaani vikali tuhuma hizo na kufunguliwa mashtaka akidai ni uchochezi wa kisiasa.