Raisi wa zamani wa marekani Donald Trump jana tarehe 4 Machi alichukua hatua ya kujisalimisha kwenda kusikiliza mashtaka yanayomkabili huko Manhattan New York.
Trump alifika mahakamani hapo majira ya mchana Kwa saa za marekani na kesi yake ilisikilizwa huku maamuzi zaidi ya kesi hiyo yakiendelea kujadiliwa.
Kutokana na wadhfa aliokuwa nao wa Raisi mstaafu, Donald Trump hatowekwa mahabusu wakati wa kesi ikiendelea, hatakiwi kufungwa pingu wala kupigwa picha ya muhalifu ‘mug shot taken”.
Katika mashtaka yanayomkabili Trump ni pamoja na kumlipa pesa haramu mwanamke alieshiriki nae kitendo cha ngono na kumtaka akae kimya hiyo inafanya awe Raisi wa kwanza kwa Taifa la marekani kushitakiwa.