ZINAZOVUMA:

Toeni mishahara mapema.

Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt...

Share na:

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameagiza malipo ya mishahara ya mwezi wa Aprili kufanyika mapema kuanzia tarehe 14 Aprili 2023 kwa wafanyakazi wa Serikali kwa ajili ya matayarisho ya Sikukuu ya Eid El Fitr.

Kwa mujibu wa tamko la Rais Dk. Mwinyi, hatua hiyo imelenga kuwapa wafanyakazi Serikalini muda wa kutosha wa kufanya maandalizi ya sherehe za Eid El Fitr.

Sherehe hizo zinatarajiwa kuangukia kati ya siku ya Ijumaa au Jumamosi ya tarehe: 21 au 22 Aprili 2023 kutokana na kuandama kwa mwezi na kuashiria mwisho wa Ramadhan.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwashukuru wafanyakazi wa Serikali kwa ushirikiano wao wakati wote wa ibada tangu kuandama kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya