Timu za Afrika Kusini Banyana Banyana na timu ya Nigeria Super Falcons zimeandika historia nyingine kwa bara la Afrika katika michuano ya kombe la dunia la wanawake huko New Zealand na Australia.
Timu hizi zimefanikiwa kuingia raundi ya 16 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa Banyana Banyana huku pia timu hiyo ikiandika historia ya kupata ushindi wake wa kwanza katika kombe la dunia.
Na kwa upande wa Nigeria ambao wanashika namba 40 duniani wanaingia hatua hii kwa mara ya tatu katika historia yao. Nigeria wameweka matatizo yao pembeni ya kudai malipo na chama cha soka nchini kwao na kuvuka kwenye kundi gumu lililokuwamo bingwa wa Olimpiki Canada.
Nigeria pia wameweka rekodi ya kuvuka hatua ya makundi bila kupoteza hata mchezo mmoja kwa mara ya kwanza.