Timu ya Taifa ya Morocco imefanikiwa kuifunga timu ya Taifa ya Brazil kwa mara ya kwanza katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki ikiwa ni mara tu baada ya wachezaji wa Morocco kufuturu.
Wachezaji wa Morocco walikua katika ibada ya funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na mara baada ya kufungua (kufuturu) ndipo mchezo huo ulichezwa.
Mchezo huo uliochezwa katika dimba la Ibn Batouta huko Morocco ulimalizika kwa Morocco kushinda magoli mawili kwa moja.
Magoli ya Morocco yalifungwa na Sofiane Boufal (29) na Abdelhamid Sabiri (78) huku kwa upande wa Brazil goli pekee likifungwa na Casemiro (67).
Morocco wameendelea kuwa na kiwango kizuri na kuweka historia katika mpira wa miguu kama walivyofanya kwenye kombe la dunia Qatar 2022.