ZINAZOVUMA:

Ten Hag kukikosa kikosi cha kwanza dhidi ya Bayern

Kocha wa Manchester United amesema kuwa hajawahi kukitumia kikosi chake...
MANCHESTER, ENGLAND - SEPTEMBER 16: Erik ten Hag, Manager of Manchester United, applauds fans following the Premier League match between Manchester United and Brighton & Hove Albion at Old Trafford on September 16, 2023 in Manchester, England. (Photo by Michael Regan/Getty Images)

Share na:

Kocha na Meneja wa Manchester United Erik ten Hag amesema hajawahi kuanzisha kikosi chake bora zaidi kutokana na wachezaji wake kukumbwa na mambo tofauti tofauti ikiwemo majeraha.

Ten Hag ameyasema hayo wakati ambao akijiandaa kukabiliana na timu ya Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa.

Ten Hag amesema wachezaji 12 wa kikosi cha kwanza watakosa mchezo huo dhidi ya mabingwa wa Bundesliga nchini Ujerumani siku ya leo jumatano.

Miongoni mwa wachezaji ambao hawatakua sehemu ya kikosi ni Pamoja na Raphael Varane, Mason Mount na Harry Maguire ambao hawajasafiri kwenda Munich.

“Siku zote kumekua na tatizo lakini lazima ushughulikie,” Ten Hag alisema.

“Nadhani sikuwahi kuanza na kikosi bora cha kwanza, hata hivyo hili ni soka unatakiwa kukabiliana nayo, Nazipenda nyakati hizi ambazo unapaswa kujua nini cha kufanya katika wakati kama huu”

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya