ZINAZOVUMA:

Tanzania yaitaka Sudan kusitisha mapigano.

Serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeitaka Sudan kusitisha...

Share na:

Serikali ya Tanzania imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano nchini Sudan yanayotekelezwa na Vikosi vya Msaada ( RSF) dhidi ya Vikosi vya Serikali nchini humo katika mji mkuu wa Khatoum na miji mengineyo ya jirani. Akiwasilisha taarifa maalum kwa Bunge kuhusu hali ya usalama nchini humo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax, amesema Tanzania inaunga mkono tamko la Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika (AU) kutaka kusitishwa kwa mapigano hayo kwa mustakabali wa ukuaji wa Sudan na Afrika kwa ujumla.

Katika hatua nyingine, Waziri Tax amebainisha kwamba jumla ya Watanzania 210, wakiwemo wanafunzi 171 na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo, hawajapatwa na madhara yoyote kufuatia machafuko hayo.

Mapigano nchini Sudan yalizuka mnamo Aprili 15, 2023 na kusitishwa kwa muda hapo jana, ili kupisha shughuli ya utoaji misaada ya kibinadamu.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya