ZINAZOVUMA:

Tanzania na Zambia yakubaliana kuhusu bomba la mafuta

Tanzania na Zambia zimekubaliana kuimarisha ulinzi katika eneo ambalo bomba...
Minister of Energy, Januari Makamba address to journalist in Dar es Salaam yesterday. Photo by Sunday George

Share na:

Mawaziri wa Nishati na Ulinzi wa Tanzania na Zambia, wamekubaliana kuimarisha ulinzi katika maeneo ambayo bomba la mafuta linalosafirisha dizeli linapita katika nchi hizo mbili.

Masuala mengine waliokubaliana ni pamoja na kuongeza idadi ya askari watakaolinda bomba hilo, kushirikiana na jamii, kutumia ndege zisizo na rubani ‘drones’ na kuongeza wigo wa bomba hilo ili lisafirishe mafuta kwa ufanisi.

Mkutano huo uliofanyika jana Julai 7, umewahusisha, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Innocent Bashungwa, wakati kwa upande wa Zambia waliwakilishwa na Waziri wa Nishati, Peter Kapala, Jacob Mwiimbu (Waziri wa Mambo ya Ndani) na Waziri wa Ulinzi, Ambrose Lufuma.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Waziri Makamba amesema wamekubaliana pia kuimarisha miundombinu ikiwemo kuongeza kambi na vituo vya polisi katika maeneo ambayo bomba hilo linapita

“Pia tumekubaliana kuimarisha kamati za ulinzi na usalama ambapo bomba linapita, matumizi ya drones na ushirikishaji wa wananchi katika vijiji,” amesema Waziri Makamba.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya