ZINAZOVUMA:

TANROADS watia kambi barabara ya Tingi – Kipatimo

Wananchi wa kipatimo wafurahishwa na juhudi za Serikali na TANROADS...

Share na:

TANROADS Mkoa wa Lindi yaweka kambi barabara ya Tingi – Kipatimo ili mawasiliano yanarudi baada ya kuharibiwa vibaya na mvua za El Nino pamoja na Kimbunga Hidaya.

Kwa pamoja majanga hayo ya asili yalisababisha baadhi ya madaraja katika barabara hiyo, kusombwa na maji na kusababisha ugumu wa kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Meneja wa Wakala TANROADS Mkoa Mhandisi Emil Zengo amesema, kambi hiyo imejikita katika kutekeleza agizo la Mheshimiwa Waziri wa ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa, aliyetaka maeneo yote yaliyoathiriwa na majanga hayo yapitike.

Eneo la kwanza lilikarabatiwa kwa kujaza kifusi katika daraja lililobebwa na maji, katika kijiji cha Mingumbi umbali wa kilomita 12.5 kutoka Tingi kwenye makutano ya barabara kuu ya Dar es Salaam kwenda Mtwara.

Harakati za kukarabati barabara ya Tingi Kipatimo zinazofanyika na TANROADS kwa Maagizo ya Serikali

Kujazwa kifusi katika eneo hilo la daraja kwa sasa kutaruhusu watu kupita, na ujenzi kuendelea katika maeneo mengine ya mbele hadi watakapomaliza.

Mhandisi msimamizi wa barabara hiyo, Fredy sanga amesema, awali barabara hiyo iliharibika kutokana na mvua za El-Nino, lakini hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya Kimbunga Hidaya.

“Mvua zilizokuja na kimbunga Hidaya zilifanya barabara kukatika maeneo mbalimbali, daraja hili lililopo Mingumbi lilikatika na kusababisha njia hii kutopitika kabisa, hivyo huduma kwa wananchi kuelekea kijiji cha Kipatimo kukosekana,” amesema Mhandisi Sanga.

Kwa upande wa Mkandarasi aliyepewa kazi ya ukarabati huo, Kasmir Shirazi Mucadam ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mucadam and Sons limited amesema, mvua ndiyo ilikuwa kikwazo katika utekelezaji majukumu yake.

“Tulisaini mkataba Machi mwaka huu lakini mvua ilikuwa changamoto, kwa sasa imetuachia na tunapambana na kazi, madaraja mengi yalibebwa na maji hayapitikiti, tunatakiwa kujaza kifusi katika eneo moja baada ya jingine hadi tunafika Kipatimo,” amesema.

Mmoja wa watumiaji wa barabara hiyo ya Tingi – Kipatimo kwa shughuli mbalimbali ikiwemo za kilimo, Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa kwa kuhakikisha fedha zinapatikana ili kunusuru kadhia wanayokumbana nayo wananchi.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia aonekana kwenye hotuba yake kupitia mitandao wiki 3

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya