ZINAZOVUMA:

Taliban yafungia vyama vyote vya siasa Afghanistan

Utawala wa Taliban imepiga marufuku vyama vyote vya siasa Afghanistan...

Share na:

Utawala wa Taliban nchini Afghanistan umepiga marufuku vyama vyote vya kisiasa nchini humo ukisema kuwa ni kinyume cha sheria za kiislamu (Shariah).

Tangazo hilo limetolewa baada ya viongozi waliochukua madaraka ya Afghanistan kuadhimisha mwaka wa pili tangu kurejesha utawala wao mjini Kabul.

Tangazo hilo limetolewa na Abdul Hakim Sharaee ambaye ni Waziri wa Sheria wa Taliban, wakati akihutubia wanahabari mjini Kabul.

Zaidi ya vyama 70 vya kisiasa vilikuwa vimesajiliwa rasmi na Wizara ya Sheria hadi pale Taliban ilipochukua udhibiti wa Taifa hilo lililokumbwa na mapigano miaka miwili iliyopita.

Tangu wakati huo, utawala huo umekuwa ukilaumiwa kuminya uhuru wa kukusanyika na kujieleza, kama mbimu ya kunyamazisha wakosoaji, wakati wafuasi wake wakiruhusiwa kuendesha shughuli zao kama kawaida.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya