ZINAZOVUMA:

Sudan yapanga kumaliza tofauti zao kurejesha amani

Baada ya mapigano ya muda mrefu nchini Sudan hatimae kikosi...

Share na:

Baada ya mapigano ya muda mrefu nchini Sudan hatimae kikosi maalum cha RSF, kimesema kinaunga mkono mpango wa usitishwaji wa kudumu wa mapigano hayo.

Hatua hiyo imeonekana kuleta matumaini ya kuwepo kwa mazungumzo ya ana kwa ana baina ya pande mbili RSF pamoja na jeshi la Sudan.

Katika taarifa yake kiongozi wa RSF Jenerali, Mohamed Hamdan Dagalo, alionekana kulegeza kamba na kuonesha utayari wa kuzungumza na utawala wa kijeshi,kwa ajili ya maslahi ya nchi ya Sudan.

Dagalo amesisitiza kuwa ni muhimu kupatikana mwafaka wa makubaliano ya amani ya kudumu yanayoambatana na suluhu ya kisiasa itakayoshughulikia pia chanzo cha mapigano hayo.

Katika mpango huo anaopendekeza Dagalo uliopewa jina la ‘Sudan Reborn’, kiongozi huyo ametaja matakwa matatu anayoamini yatasaidia kumaliza mzozo huo ambayo ni uongozi unaoheshimu utafauti wa makabila,jeshi moja na uchaguzi wa demokrasia.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya