Serikali ya Somalia imeingia makubaliano ya kupeleka matunda nchi Ethiopia.
Nchi hizo mbili zimeingia makubaliano hayo wiki iliyopita, lengo likiwa ni kudhibiti uingizaji haramu wa bidhaa nchini Ethiopia.
Pia makubaliano hayo yanatarajiwa kupunguza hata uingizaji haramu wa wanyama kutoka Somalia.
Makubaliano hayo yamekusudia kuchagua bidhaa za kuuziana kutoka pande hizo mbili.
Waziri wa biashara na ushirikiano wa kikanda wa Ethiopia Bw. Gebremeskel Chala amesema kuwa “Lengo la makubaliano hayo ni kukuza manufaa ya nchi zote mbili katika biashara”.
Pamoja na bidhaa zote zilizoainishwa katika makubaliano hayo, Miraa imechukua nafasi kubwa kama bidhaa ya kupeleka Somalia kutoka Ethiopia.
Huku waziri huyo akisema kuwa wenzao wa Kenya wamewapiku mno katika kuingiza Miraa Somalia, huku wakulima wa miraa nchini Ethiopia wakihangaika kungiza kwa magendo mizigo yao ya miraa.