ZINAZOVUMA:

Waziri Mkuu atoa maagizo kwa Dkt Biteko kuhusu mafuta

Waziri Mkuu amemuagiza Naibu Waziri Mkuu kuhakikisha anashughulikia suala la...

Share na:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Dotto Biteko kushughulikia suala la upatikanaji mafuta nchini na kuhakikisha ndani ya wiki moja majibu yanapatikana na taarifa itolewa kwa Watanzania.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo bungeni leo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu.

Mbunge huyo alihoji mkakati wa serikali kutokana na sintofahamu ya upatikanaji wa mafuta katika vituo mbalimbali vya kuuza nishati hiyo hivi karibuni.

Ambapo amesema mafuta ya petrol na disel yamekuwa hayapatikani katika baadhi ya maeneo, lakini bei ikishatangazwa yananza kupatikana, lakini pia alizungumzia suala la bei ya mafuta kubadiika mara kwa mara

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema ni kweli kuna changamoto ya upatikanaji mafuta nchini, ambapo baadhi ya vituo maeneo kadhaa vilikuwa havina mafuta na kwamba serikali inafanya jitihada mbalimbali kutatua tatizo hilo kuanzia Wizara ya Nishati na hata Kamati ya Bunge ya Nishati wamekaa mara kadhaa kwa ajili ya jambo hilo.

Hata hivyo amesema kutokana na mabadiliko aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni kwa kumteua Dkt Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, ameonekana mara kadhaa Dkt Biteko akifanya vikao mbalimbali na wadau wa masuala ya mafuta, hivyo amemuagiza kushughulikia suala hilo na likipatiwa ufumbuzi ndani ya wiki moja taarifa itatolewa.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya