ZINAZOVUMA:

Simba wapungua kwa 45% nchini Uganda

Waziri wa Utalii nchini Uganda akiri kupungua kwa Simba nchini...

Share na:

Uganda inakabiliwa na upungufu mkubwa wa idadi ya simba kufuatia kupungua kwa asilimia 45 kwa wanyama hao katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, wizara ya utalii na wanyamapori ilisema Jumanne.

Idadi ya wanyama hao wanaochukuliwa kama wafalme wa nyika ilipungua kutoka 493 hadi 275, kutokana kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa mzozo kati ya binadamu na wanyamapori, wizara hiyo ilisema.

“Simba walipingua sana kutokana na mauaji ya kulipiza kisasi, yanayosababishwa na mzozo kati ya binadamu na wanyamapori,” waziri Tom Butime alisema alipokuwa akitoa ripoti ya utalii nchini humo.

“Idadi ya simba ilipungua kutoka 493 mwaka 2014 hadi 275 mwaka 2023.”

Hata hivyo, Butime alisema anafuraha kutangaza kwamba idadi ya baadhi ya viumbe imeongezeka, wakiwemo sokwe, ambao idadi ilitoka 302 mwanzoni mwa mwaka wa 2000 hadi 452 ifikapo 2022.

Uganda ina sifa ya kuwa moja ya nchi yenye viumbe vingi hai duniani.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya