ZINAZOVUMA:

Siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani

Leo Mei 03 ni siku ya uhuru wa vyombo vya...

Share na:

Leo ni maadhimisho ya miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayoadhimishwa Mei 03 kila mwaka, ambapo kitaifa mwaka huu yanafanyika Zanzibar.

Katika maadhimisho hayo Baraza la Habari Tanzania (MCT) limesema katika kipindi cha miaka 10 tangu mwaka 2012 wandishi wa habari 272 wamekumbwa na madhila tofauti kazini ikiwemo ajali, kupigwa, kunyang’anywa vifaa vya kazi, kutekwa na kuuawa.

MCT imesema taasisi inayoongoza kwa matukio mengi dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari ni polisi yenye matukio 51, ikifuatiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yenye matukio 21.

Aidha kwa upande wake Balozi wa Marekani Nchini Tanzania, Michael Battle amesema uhuru wa maoni na uhuru wa habari ni msingi wa haki nyingine za binadamu.

“Tunatambua umuhimu wa wanahabari. Watu wote wana haki ya kutafuta ukweli na kuusema bila kuwa na hofu ya kuumizwa Kihisia, Kiuchumi, Kifedha au Kiakili. Vivyo hivyo kwa Vyombo vya Habari, vina haki ya kutafuta habari”

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya