Mfanyabiashara maarufu wa Qatar Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani amefanya maboresho ya ofa yake ili aweze kuinunua klabu ya soka ya Manchester United.
Vyanzo vya habari vinasema kwamba dau jipya liliwasilishwa jana Jumanne asubuhi huku mazungumzo yakifanyika na Raine Group, ambao ndio wanaoshughulikia mauzo ya klabu hiyo.
Mfanyabiashara huyo wa Qatar ambaye ni mwekezaji katika benki pamoja na Sir Jim Ratcliffe’s Ineos Group ambazo ndizo pande mbili kuu zinazotazamia kuinunua klabu hiyo ya Old Trafford.
Makundi hayo yote mawili yaliwasilisha dau la tatu mwishoni mwa mwezi Aprili.
Inafahamika kuwa dau jipya ambalo ni kwa ajili ya kuinunua 100% ya klabu , litalipa deni lote na kujumuisha pesa nyingine ambazo zitaelekezwa moja kwa moja katika klabu na shughuli za kijamii za eneo la klabu.