ZINAZOVUMA:

Sheikh afia gerezani akitumikia kifungo cha maisha

Sheikh Delwar Hossain Sayeedi amefariki akiwa gerezani akitumikia kifungo cha...

Share na:

Sheikh na Mwanazuoni Mkubwa kutoka nchini Bangladesh Delwar Hossain Sayeedi amefariki dunia akiwa gerezani akitumikia kifungo cha maisha jela.

Sheikh Delwar alikamatwa mwaka 2010 na kuhukumiwa kifo kutokana na makosa ya kihalifu aliyokutwa nayo, lakini mwaka 2014 alibadilishiwa adhabu na kupewa kifungo cha maisha jela.

Mamlaka za kutetea haki za binadamu zimelaani tukio hilo huku wakitaka sheria za hukumu ya kifo iangaliwe upya nchini humo.

Sheikh Delwar alifariki kutokana na mshutuko wa moyo akiwa katika gereza la Kashimpur huko Bangladesh.

Toka mwaka 2010 ameitumikia kifungo chake gerezani mpaka umauti ulipomfika akiwa mzee wa miaka 83.

Watu mbalimbali na waumini wakiislamu wameandamana kulaani serikali ya Bangladesh lakini wakianikiza kuutaka mwili wa sheikh huyo ili waweze kwenda kuzika.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,