ZINAZOVUMA:

Serikali yahakikishiwa uwepo wa mafuta

Serikali yahakikishiwa uwepo wa mafuta na wamiliki wa maghala baada...

Share na:

Wamiliki wa maghala ya mafuta nchini wameihakikishia Serikali kuhusu upatikanaji wa mafuta wakisema kuwa wana petroli na dizeli za kutosha na wapo tayari kutoa ushirikiano wa kuyasambaza kwenye maeneo mbalimbali yenye uhitaji.

Wadau wameiambia Serikali kuwa hivi sasa wanafanya kazi saa 24 hadi siku za mapumziko ili kuhakikisha magari yanaingia na kutoka katika maghala kwa lengo la kuchukua mafuta na kuyasafirisha katika maeneo mbalimbali.

Wametoa hakikisho hilo jana Jumapili Julai 23, 2023 mbele ya Waziri wa Nishati, January Makamba aliyeambatana Kamishna wa Mafuta na Gesi Asilia, Michael Mjinja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Dk James Andilile.

Hii ni mara ya pili kwa Ewura kukagua na maghala hayo na kuzungumza na wamiliki kuhusu hali ya upatikanaji wa mafuta katika maeneo mbalimbali baada ya hivi karibuni kuzuka sintofahamu kwa baadhi ya maeneo kutopata nishati hiyo kwa uhakika.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya