ZINAZOVUMA:

Serikali yaboresha jeshi la zimamoto na uokoaji.

Serikali imezindua kituo kipya cha zimamoto na uokoaji Dodoma na...

Share na:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Aprili 26, 2023 amezindua kituo cha kisasa cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Nzuguni, jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya miradi inayozinduliwa katika juma la kilele cha maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Waziri Mkuu amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani imeendelea kutekeleza dhamira yake ya kufanya maboresho makubwa ya kiutendaji pamoja na ujenzi wa miundombinu muhimu ya Jeshi la zimamoto.

Aidha ameweka wazi kuwa Serikali itafanya ununuzi wa magari 5 ya kuzima moto na uokoaji, itakarabati nyumba 10 za makazi ya maafisa na askari wa jeshi la zimamoto pamoja na ujenzi wa miundombinu ya chuo cha zimamoto na uokoaji Chogo kilichopo wilayani Handeni Tanga.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya