Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, amelazwa hospitali baada ya kugomea kula chakula kwa muda, katika kile alichokisema ni hatua ya kupinga mashtaka yake anayotuhumia na serikali ya nchi hiyo.
Kiongozi huyo ambaye chama chake cha PASTEF kilifungiwa wiki iliyopita alifunguliwa mashatka ya kuchochea uasi, kula njama dhidi ya serikali na masuala mengine ya kihalifu.
Katika hatua ya kupinga mashtaka hayo yenye lengo la kumdhoofisha kwenye uwanja wa siasa Sonko alianza mgomo wake wa kususia kula akiwa gerezani hali iliyopelekea kulazwa kwake.
Chama chake kilichofungiwa kinailaumu serikali ya Senegal kwa hali anayopitia Sonko hivi sasa na kimeweka wazi kuwa alikua mzima wa afya hapo awali na kama kuna lolote litakalomkuta basi mamlaka itakua na la kujibu.