ZINAZOVUMA:

Serikali ya Kenya yarudisha ruzuku ya mafuta

Serikali nchini Kenya imebadilisha msimamo wake na kuuamua kurudisha ruzuku...

Share na:

Serikali ya Kenya imebadilisha msimamo wake na kurudisha ruzuku ya mafuta huku ikiangazia kuwakinga raia wake dhidi ya bei ya juu ya bidhaa hiyo.

Shirika la Udhibiti wa Mafuta nchini Kenya, EPRA halikubadilisha bei ya bidhaa hiyo baada ya kurudisha ruzuku hiyo ambapo bei ya mafuta ilitarajiwa kupanda hadi ksh 200 kwa lita moja ya petroli.

‘’Ili kuwalinda wateja dhidi ya kupanda kwa bei ya mafuta , serikali imeamua kudhibiti bei ya mafuta katika kipindi cha mwezi Agosti na Septemba’’ , ilisema EPRA katika taarifa yake.

EPRA imesema kwamba kampuni za mafuta zitafidiwa kutoka katika hazina ya Mafuta ya nchi.

Kwa mujibu wa EPRA, bei ya mafuta ingepanda hadi kufikia 202 kwa lita ya petroli huku dizeli ingeuzwa kwa ksh.183.26 kwa lita na kwa mafuta ya taa yangepanda hadi ksh.175.22 kwa lita jijini Nairobi.

Lakini sasa bei ya bidhaa hiyo itasalia kuwa Ksh.194.68 kwa lita ya petroli, Ksh.179.67 kwa lita ya dizeli, na Ksh.169.48 kwa lita ya mafuta taa.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya