ZINAZOVUMA:

Serikali ya Kenya yamuondolea ulinzi Raila Odinga

Serikali ya Kenya imemuondolea ulinzi kiongozi wa upinzani Raila Odinga...

Share na:

Serikali ya Kenya imemfutia ulinzi kiongozi wa upinzani Raila Odinga na kuwaondoa walinzi wake wote pamoja na wale waliokuwa wakilinda makazi yake.

Uamuzi huo wa kuwaondolea ulinzi wapinzani hao, umekuja muda mfupi baada ya kiongozi huyo kuwatangazia Wananchi kuwa wajiandae kwa Maandamano ya Kimapinduzi kuanzia Julai 19, 2023, Maandamano ambayo yamepata pia kibali cha Mahakama.

Kwa mujibu wa taarifa, Askari 10 wanaomlinda Odinga na wengine wanaolinda Makazi yake jijini Nairobi, Kisumu na Siaya wameondolewa pamoja na walinzi wanaowalinda Wabunge zaidi ya 50 wa upinzani.

Wengine waliofutiwa ulinzi ni mwanasiasa Kalonzo Musyoka na Magavana wanne.

Aidha Jana Julai 17, 2023 Mahakama Kuu ilifutilia mbali ombi la zuio la Maandamano hayo na kueleza kuwa ni Haki ya kikatiba.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya