ZINAZOVUMA:

Serikali kuongeza huduma ya mawasiliano

Serikali inaenda kuongeza minara yenye uwezo wa kutoa huduma ya...

Share na:

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba amesema serikali inaenda kuongeza uwezo wa minara 304 kutoa huduma ya teknolojia ya 3G na 4G katika maeneo mbalimbali nchini.

Justina amesema minara hiyo ilikuwa ikitoa huduma ya teknolojia ya 2G hapo awali.

Amezungumza hayo katika hafla ya utiaji saini mikataba ya kupeleka huduma ya mawasiliano nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo, Mei 13.

Katika Hafla hiyo iliyohudhuriwa na Raisi Dkt Samia Suluhu Hassani, Kampuni tano za mawasiliano nchini zimesaini mkataba na serikali kupeleka mawasiliano ya mnara katika vijiji 1,407 vya Tanzania Bara.

Kampuni hizo ni Vodacom Tanzania, Tigo, Airtel, TTCL na Halotel.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya