ZINAZOVUMA:

Sakho apewa mkono wa kwaheri na Simba

Klabu ya Simba imetangaza kuachana na mchezaji wake raia wa...

Share na:

Klabu ya Simba imetangaza rasmi kumuuza kiungo wao mshambuliaji, Pape Sakho kwa klabu ya Quevilly Rouen Metropole inayoshiriki daraja la pili nchini Ufaransa.

Sakho raia wa Senegal ameichezea Simba kwa misimu miwili akipata mafanikio mbalimbali ikiwemo kushinda bao bora la michuano ya CAF pamoja na kuitwa kikosi cha Taifa Senegal.

Aidha Simba imefanya usajili wa golikipa kutoka nchini Brazil ambae atakuja kuchukua nafasi ya golikipa wao namba moja Aishi Manula ambae ni majeruhi kwa sasa.

Mchezaji huyo amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia miamba hiyo ya soka nchini Tanzania.
Taarifa zinasema kuwa kipa huyo lilikua ni pendekezo la kocha Mkuu wa Simba Robertinho.

Simba imeendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa 2023/2024 ambapo licha ya usajili mkubwa uliofanywa wamefanikiwa pia kumrudisha mchezaji wao Luis Miquissone akitokea klabu ya Al Ahaly walipomuuza misimu miwili iliyopita.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya