ZINAZOVUMA:

Ramaphosa aijibu Marekani kuhusu kuisaidia Urusi

Raisi wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameijibu Marekani baada kushutumiwa...

Share na:

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amejibu madai ya Marekani ya kuishtumu nchi yake kuwa ilitoa silaha kwa Urusi licha ya msimamo wake kwamba haiegemei upande wowote katika vita vya Urusi na Ukraine

Rais Ramaphosa amesema serikali yake inachunguza madai hayo na hata hivyo nchi yake imesimamia madai ya kutoegemea upande wowote katika uvamizi wa Ukraine.

Mamlaka ya Afrika Kusini ilikanusha kuwa ushirikiano wa mazoezi ya kijeshi uliwekwa ili kuendana na kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kuanza kwa vita na kusema kuwa nchi hiyo mara kwa mara huwa na mazoezi kama hayo na mataifa mengine, ikiwa ni pamoja na Ufaransa na Marekani.

Awali Afrika Kusini haikupiga kura ya Umoja wa Mataifa kulaani uvamizi huo, pia ilikataa kuungana na Marekani na Ulaya katika kuiwekea Urusi vikwazo.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya