ZINAZOVUMA:

Ramaphosa: Afrika Kusini haifungamani na upande wowote

Raisi wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema nchi yake haitafungamana...

Share na:

Raisi wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema kuna “shinikizo la ajabu” kwa nchi hiyo kuacha msimamo wake wa kutofungamana na upande wowote kuhusu vita vya Ukraine.

Katika taarifa yake Raisi Ramaphosa amesema Afrika Kusini haitaunga mkono upande wowote katika kile alichosema ni “mashindano kati ya Urusi na Magharibi”.

Kauli yake inakuja siku chache baada ya balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, Reuben Brigety, kuishutumu nchi hiyo kwa kutoa silaha na risasi kisiri kwa Urusi, licha ya kudai kutoegemea upande wowote.

Balozi Brigety alisema ujasusi wa Marekani ulikuwa na uhakika kuwa silaha zilikuwa zimepakiwa kwenye meli ya Urusi katika kambi ya wanamaji mjini Cape Town.

Ramaphosa amekubali kuchunguza madai hayo lakini anasema hakuna ushahidi thabiti wa kuunga mkono madai hayo.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya