Raisi wa Gabon Ali Bongo Ondimba ametangaza kuwa atawania muhula wa tatu wa uchaguzi wa raisi unaotarajiwa kufanyika Agosti 26, 2023.
Wakati akitangaza azma yake ya kuwania tena urais wa Gabon Rais Bongo amesema ana ndoto ya kuibadilisha Gabon.
“Tutaifanya na tunaweza kuifanya Gabon kuwa taifa imara, taifa bora na sehemu bora ya kuishi. Hii ni azma yangu, azma ambayo haijashindwa kunisukuma na inaendelea kunipa msukukumo kila siku. Naweza kukosolewa kwa mengi lakini sio kukosa ari na ndoto kwa ajili ya taifa langu nnanifahamu kwangu kutowezekana sio neno nilijualo”
Katika uchaguzi uliopita uliofanyika mwaka 2016 ulikumbwa na madai ya udanganyifu wa kura ambapo Rais Bongo alimshinda aliyekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Jean Ping.
Hata hivyo kiongozi huyo wa Gabon anashutumiwa kwa kuukandamiza upinzani katika uongozaji wake.
Aidha Bwana Bongo mwenye umri wa miaka 64 alichukua madaraka mwaka 2009 kutoka kwa baba yake Omar Bongo ambaye aliiongoza Gabon kwa zaidi ya miaka 40 tangu mwaka 1967 hadi alipofariki dunia.
Gabon haina ukomo wa mihula ya kugombea kuambatana na katiba ya taifa hilo lenye utajiri wa mafuta.