ZINAZOVUMA:

Raisi Samia aunda wizara mpya

Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu...

Share na:

Kufuatia kutungwa kwa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na uamuzi wa kuhamishia masuala ya uwekezaji Ofisi ya Rais, hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Miundo ya Wizara na kufanya uteuzi wa viongozi katika nafasi hizo.

Rais Samia ameunda wizara ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji ambapo amemteua Prof. Kitila Alexander Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji. Mhe. Prof. Mkumbo ni mbunge wa jimbo la Ubungo.

Raisi Samia Ameunda Wizara ya Fedha ambapo amemteua Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck
Nchemba kuwa Waziri wa Fedha. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Dkt. Nchemba alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Ameunda Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo amemteua Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa wizara hiyo. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Dkt. Kijaji alikuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Amemteua Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Taifa. Kabla ya uteuzi huu Bw. Mafuru alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango (Usimamizi wa Uchumi).

Amemteua Bw. Elijah Mwandumbya kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (Usimamizi wa Uchumi). Kabla ya uteuzi huu Bw. Mwandumbya alikuwa Kamishna, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya