Raisi wa Cameroom Paul Biya amefanya mabadiliko katika Wizara ya Ulinzi na kuwateua viongozi wapya wa kijeshi mara baada tu ya mapinduzi yaliyofanyika nchini Gabon.
Biya ni mmoja wa marais waliokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika. Hakuna sababu iliyotolewa kuhusu hatua hiyo ya mabadiliko hayo makubwa ya ghafla yaliyofanyika
Hata hivyo Kanali Cyrille Guemo, Mkurugenzi wa mawasiliano katika Wizara ya Ulinzi ya Cameroon, amesema kwamba uteuzi huo mpya ulikua kwenye mipango ya Rais kwa siku nyingi.
Lakini kutokana na hali ya mapinduzi ya kijeshi ambayo yanaenea katika mataifa ya Afrika Magharibi, viongozi ambao wamekuwa madarakani kwa muda mrefu sana wameingiwa na wasiwasi.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamesema kizazi cha vijana ambacho kinaundwa na viongozi wa kijeshi hakivumilii tawala zinazofanya kazi kutakana na nasaba zao.