ZINAZOVUMA:

Rais Samia amuondoa Chande TTCL na kumpeleka Posta

Raisi Samia Suluhu Hassani amefanya mabadiliko na uteuzi mbalimbali huku...

Share na:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na mabadiliko katika nafasi mbalimbali.

Raisi Samia amemteua Bw. John Ulanga kuwa Balozi, Bw. Ulanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Raisi Samia ameivunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na amemteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Gideon Kingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Aidha amemteua Bw. Maharage Chande kuwa Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Chande aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) akitokea Shirika la Umeme Tanzania TANESCO.

Bw. Chande anachukua nafasi ya Bw. Macrice Daniel Mbodo ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Aidha, Mhandisi Peter Ulanga ataendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Uteuzi huu unaanza mara moja na Balozi Mteule Bw. Ulanga ataapishwa tarehe 26 Septemba, 2023 Ikulu, Dar es Salaam.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya