ZINAZOVUMA:

Rais Mnangagwa adhinda urais Zimbabwe

Raisi wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amefanikiwa kutetea kiti chake cha...
Zimbabwean President and ZANU PF leader Emmerson Mnangagwa (C) raises his cap in salute to the crowd gathered during a rally in Harare on August 9, 2023. (Photo by Jekesai NJIKIZANA / AFP)

Share na:

Tume ya Uchaguzi nchini Zimbabwe ZEC imemtangaza Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kutoka Chama cha ZANU-PF kuibuka mshindi katika uchaguzi Mkuu kwa asilimia 52.6 ya kura zote.

Akisoma matokeo ya uchaguzi mkuu Mwenyekiti wa ZEC Justice Chigumba amesema Mnangagwa alipata zaidi ya kura milioni 2.3 ilhali mpinzani Mkuu ambaye ni mgombea wa Chama cha Wananchi (CCC) Nelson Chamisa, alipata zaidi ya kura milioni 1.9 ambayo ni sawa na asilimia 44 ya kura zote.

Akizungumzia kuhusu matokeo hayo Rais Mnangagwa amewashukuru wote walioshiriki katika uchaguzi huo na kusema hakuna aliyeshindwa wala aliyeshinda isipokuwa lengo la pamoja ni kujenga taifa imara la Zimbabwe.

“Tutabaki milele kuwa watu wa umoja, wapenda amani na wastahimilivu, kutoka Zambezi hadi Limpopo, Plumtree hadi Mutare, tukiimba kwa fahari wimbo mmoja wa taifa, chini ya bendera moja ya taifa. Naomba nitoe pongezi kwa makanisa yetu yote kwa kuendeleza amani na utangamano” Amenukuliwa Mnangagwa.

Hii ni awamu ya pili kwa Mnangagwa maarufu ‘The crocodile’ kushika nafasi hiyo ambapo kwa mara ya kwanza aliingia madarakani 2017 kufuatia vuguvugu la siasa lililomuengua aliyekuwa Rais na baba wa taifa hilo hayati Robert Mugabe.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya