ZINAZOVUMA:

Putin aapishwa kwa muhula wa tano

Rais Putin wa urusi kuapishwa tena jijini Kremlin kushika wadhifa...

Share na:

Vladimir Putin aapishwa kwa muhula wake wa tano kama Rais wa Urusi siku ya Jumanne, na kufuatiwa na sherehe ya kumpongeza jiji Kremlin wakati jeshi lake likiendelea kusonga mbele katika vita vya Ukraine.

Putin mwenye umri wa miaka 71 alirefusha utawala wake nchini humo kwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi mwezi Machi.

Baada ya kupambana kushikilia madaraka na taifa hilo kubwa duniani kwa robo karne, Putin aliweka tena mkono wake juu ya katiba ya Urusi kwenye sherehe ya Jumanne na kuapa kuwatumikia watu wa Urusi katika muhula wake wa tano wa urais.

“Sisi ni watu wa umoja na wakubwa na kwa pamoja tutashinda vikwazo vyote, tutambue mipango yetu yote. Kwa pamoja tutashinda!” alisema baada ya kuapishwa mbele ya ukumbi mkubwa uliojaa vigogo.

Taifa hilo ambali hadi sasa linaaminika kukandamiza upinzani ndani ya nchi na kuwa ndio sababu ya vita vya Ukraine, lipo katika vikwazo vya kidunia kutoka nchi mbalimbali duniani.

Hata hivyo mbali na kutengwa, bado mataifa ya ulaya yameendelea kununua nishati ya gesi kutoka Urusi, ili kupunguza makali ya msimu wa baridi uliopita kuanzia Disemba hadi Februari barani ulaya.

Nchi nyingi za Magharibi zilisusia sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Putin, ambapo umefanyika siku chache baada ya Putin kuruhusu kufyatuliwa silaha za nyuklia.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,