ZINAZOVUMA:

Putin aahidi kulipa kisasi baada ya shambulio la Crimea

Raisi wa Urusi Vladimir Putin ameahidi kulipiza kisasi kwa Ukraine...

Share na:

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameapa kulipiza kisasi kwa Ukraine kutokana na shambulio jipya la ndege mbili zisizo na rubani za Ukraine kwenye daraja la Crimea.

Rais Putin alisema wakati akizungumza na maafisa wa kijeshi kuwa hatua sahihi kwa sasa zinapimwa na Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo ili kuona hatua itakayochukuliwa.

“Tukio hilo ni shambulio lingine la kigaidi la serikali ya Kiev, uhalifu huu hauna maana kwa mtazamo wa kijeshi, kwani daraja la Crimea kwa muda mrefu halijatumika kwa usafiri wa kijeshi, na ni la kikatili kwani ni raia wasio na hatia tu waliuawa na kujeruhiwa,” Rais Putin alisisitiza.

Putin alisema Moscow italipiza kisasi kwa shambulio hilo na tayari Wizara ya Ulinzi ya Urusi inatayarisha mapendekezo kwa hatua kama hizo.

Aidha Rais Putin aliwataka maafisa kuimarisha ulinzi karibu na daraja hilo akibainisha kuwa hilo ni pigo la pili dhidi yake.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya