ZINAZOVUMA:

Prigozhin amuweka matatani Putin

Prigozhin mrusi na swahiba mkubwa wa Putin awa mwiba wenye...

Share na:

Founder of Wagner private mercenary group Yevgeny Prigozhin in Moscow, Russia, in a file photo taken on April 8 2023. Picture: REUTERS/YULIA MOROZOVA

Rais Vladimir Putin aliwapongeza wanajeshi na vikosi vya usalama vya Urusi katika hafla maalum baada ya jaribio lililoshindwa la uasi lililoongozwa na kiongozi wa kikundi cha Wagner, Yevgeny Prigozhin. Putin aliwaambia walinzi wa usalama zaidi ya 2,500 waliokusanyika katika eneo la Kremlin kwamba wananchi na vikosi vya jeshi walikuwa pamoja kupinga wapiganaji waasi.

Putin pia aliomba ukmya wa dakika moja kuwaheshimu marubani wa kijeshi wa Urusi waliouawa wakati wa uasi. Ingawa waasi walishambulia ndege kadhaa walipokuwa wakikaribia Moscow, hawakukabiliana na upinzani wa ardhini. Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu alikuwepo katika sherehe hiyo, ambapo kufutwa kazi kwake kulikuwa moja ya madai makuu ya waasi.

Prigozhin, mshirika wa zamani wa Putin na mfungwa aliyekuwa na vikosi vyake vya kijeshi ambavyo vimepambana kwa niaba ya Urusi katika vita vya Ukraine na hata Syria. Prigozhin  alisema amepata mwaliko wa Alexander Lukashenko Rais wan chi jirani ya Belarus, ambaye pia ni mshirika wa karibu wa Putin. Maelezo ya safari yake ya uhamishoni hayakuwa wazi kwa umma na hakukuwa na uthibitisho wa mahali alipo  kiongozi huyo siku tatu tangu uasi huo kutokea, pia haifahamiki kama kweli alikuwepo katika ndege iliyofuatiliwa ikielekea Belarus Jumanne asubuhi.

Ndege iliyohusishwa na Prigozhin ilifika Belarus kutoka Urusi, ikiaminika kumleta kiongozi huyo wa wapiganaji wa Wagner uhamishoni, siku tatu baada ya kusitisha ghafla uasi wake huku wapiganaji wake wakikaribia mji mkuu wa Moscow. Mamlaka zimeripoti kuwa kesi ya uhalifu dhidi ya kikundi cha Wagner imesitishwa, ikikidhi mojawapo ya masharti ya makubaliano yaliyofikiwa Jumamosi usiku ambayo yalikuwa chachuya kusuluhisha mzozo huo.

Tovuti ya huduma ya kufuatilia ndege ya Flightradar24 ilionyesha ndege aina ya Embraer Legacy 600, yenye nambari za utambulisho zinazoshabihiana na ndege inayohusishwa na Prigozhin kwenye nyaraka za vikwazo vya Marekani. Ndege hiyo inaaminika kuwa ilianza safari Rostov nchini urusi mji ulokuwa chini ya wapiganani wa Wagner na ilishuka Minsk, mji mkuu wa Belarus.

Prigozhin alionekana mara ya mwisho hadharani Jumamosi usiku, akicheka na kuwapungia mkono watu waliokuwa pembeni yake alipokuwa akiondoka Rostov ndani ya gari baada ya kuamuru wapiganaji wake kuacha uasi.

Putin alisema katika hotuba yake kupitia runinga Jumatatu usiku kwamba viongozi wa uasi walitenda usaliti kwa nchi yao, bila kumtaja Prigozhin kwa jina. Alisema wapiganaji wa Wagner wataruhusiwa kujiunga na jeshi la Urusi, kuweka makazi yao nchini Belarus au kurudi nyumbani.

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, alisema katika mkutano na waandishi wa habari Jumanne kwamba makubaliano ya kumaliza uasi yanatekelezwa, na hana taarifa juu ya mahali alipo Prigozhin. Alisema pia hajui idadi ya wapiganaji wa Wagner watakaosaini mikataba na Wizara ya Ulinzi. Huku akimalizia kwa kusema kuwa ni kicheko kuhisi kuwa mamlaka ya Putin yametetereka kutokana na uasi uliotokea.

Chanzo: Reuters

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya