ZINAZOVUMA:

Polisi Tanzania kushiriki mafunzo na nchi nyingine 14

Polisi Tanzania kuwa mwenyeji wa mafunzo ya pamoja kwa nchi...

Share na:

Jeshi la Polisi Nchini, limesema linatarajia kuwa, mwenyeji mafunzo ya utayari kwa vitendo (Field Training Exercise – FTX) mwaka huu kuanzia Aprili 13 hadi Aprili 18, 2024.

Mafunzo hayo yatajumuisha vikosi vya polisi vya nchi 14 kutoka Afrika, nchi zote zitakazoshiriki ni wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Ukanda wa Mashariki mwa Afrika (EAPCCO).

Taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji wa Polisi leo Aprili 11, 2024 aibu Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime imesema kuwa tukio linatarajiwa kufanyika katika Chuo Cha Polisi (CCP) – Moshi.

Na linatarajiwa kuhudhuriwa maaskari 670 wakiwemo Maafisa, wakaguzi pamoja na askari wengine wa vyeo mbalimbali.

DCP Misime amebainisha kuwa kufanyika kwa mazoezi hayo kunatokana na maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa Shirikisho hilo la wakuu wa polisi Ukanda wa Mashariki katika mikutano yao ya kila mwaka.

Ameongeza kuwa katika mkutano uliofanyika mwezi Oktoba, 2021 mjini Kinshasa nchini Kongo, wakuu hao wa polisi walipitisha azimio la zoezi hili kufanyika hapa nchini.

Taarifa hiyo ya Msemaji pia imezitaja nchi zinazotarajiwa kushiriki ni Tanzania kama mwenyeji, Burundi, Eritrea, Djibouti, DRC Kongo, Kenya, Comoro, Ethiopia, Shelisheli, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudani Kusini pamoja na Uganda.

Msemaji wa Jeshi hilo amebainisha kuwa lengo la mafunzo hayo na mazoezi mengine yaliyopita ni kuwajengea Maofisa wa vikosi vya polisi kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu unaovuka mipaka na kubadilishana uzoefu na taarifa za kitelejensia.

Uhalifu unaolengwa ni kama vile ugaidi, usafirishaji haramu wa binadamu, biashara haramu ikiwemo dawa za kulevya.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya