ZINAZOVUMA:

AL HILAL ya Sudan kuomba kucheza ligi ya NBC

Al Hilal yaomba kukichafua ligi kuu ya Tanzania maarufu kama...

Share na:

Baada ya wanafunzi wa Udaktari kutoka Sudan kuvinjari mitaa ya muhimbili, timu nguli ya mpira wa miguu barani Afrika kutoka AL HILAL nayo imeomba kucheza ligi kuu ya Tanzania.

Hii ni kutokana na kusimama kwa ligi ya Sudan kwa sababu ya vita za wenyewe kwa wenyewe zinaondelea huko nchini humo.

Baada ya kuona hakuna muelekeo wa mapigano hayo kusimama hivi karibuni, yimu hiyo imeomba kucheza ligi ya NBC ya Tanzania kama mbadala ili kujiweka sawa.

Taarifa kuyoka vyombo vya kuaminika imesema kuwa klabu ya hiyo imetuma barua kwa TFF kuomba kucheza ligi kuu ya NBC ili kujiweka sawa na kuamini kuwa ligi hii ni sahihi kwa wao kutokana na ubora wa ligi ya Tanzania, Afrika. Kama AL HILAL itakubaliwa basi italeta ushindani mkubwa kwa Simba na Yanga na kuimarisha ligi yetu zaidi.

Watanzania mko teyari kuwapokea AL HILAL.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya