ZINAZOVUMA:

Sudan yagomea mkutano wa kutafuta amani

Serikali ya Sudan imegoma kushiriki mkutano wa kikanda wa kutafuta...

Share na:

Serikali ya Sudan imekataa kushiriki katika mkutano wa kikanda wenye lengo la kumaliza miezi mitatu ya mapigano ya kikatili huku ikiishtumu Kenya ambayo inasimamia mazungumzo hayo kuwa inapendelea kikosi hasimu cha wapiganaji.

Mapambano hayo ya madaraka kati ya mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdan Dagalo, kamanda wa kikosi cha dharura (RSF), yalizuka katikati ya mwezi Aprili na tangu wakati huo, yameua maelfu ya watu na kulazimisha mamilioni ya wengine kuhama makazi yao.

Jumuia ya nchi za Afrika Mashariki (IGAD) jana Jumatatu iliwaalika mahasimu hao kwenye mkutano katika mji mkuu wa Ethiopia, huku mapigano yakizidi kupamba moto kote nchini Sudan.

Si Burhan wala Dagalo aliyehudhuria mazungumzo hayo mjini Addis Ababa, ingawa kikosi cha RSF kilituma mwakilishi wake kwenye mkutano wa nchi nne uliongozwa na Kenya, Sudan Kusini, Djibouti na Ethiopia.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya