ZINAZOVUMA:

70 wafariki kwa surua Sudan Kusini

Watoto zaidi ya 70 wamepoteza maisha nchini Sudan Kusini kutokana...

Share na:

Watoto zaidi ya 70 wamepoteza maisha kwa kipindi cha wiki tatu zilizopita nchini Sudan Kusini, kutokana na ugonjwa wa Surua.

Aidha watalaam wa afya wanaonya kuwa iwapo watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, hawatopata lishe nzuri, itakayowasaidia kujikinga na ugonjwa huo, hali itaendelea kuwa mbaya zaidi.

Wizara ya Afya nchini humo inasema tangu kuanza kwa mwaka huu, ugonjwa huo umekuwa ukiripotiwa mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Daktari Abdallah Faheem kutoka jimboni Jonglei amesema kwamba ‘‘Ugonjwa wa surua umezuka katika maeneo kadhaa nchini humo na Surua ilipozuka imesababisha magonjwa mengine kama kuharisha ambayo yanaweza kutokea kwa mgonjwa wa surua”.

“Mtoto anaweza kupata ugonjwa wa nimonia akiwa na Surua, vilevile Surua inaambukizwa na kuenezwa haraka kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine”.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya